CAF CL: Mlipili kuanza dhidi ya Gendamarie

Kocha mkuu wa kikosi cha Simba SC, Pierre Lechantre hajafanya mabadiliko yoyote katika kikosi ambacho kitaanza dhidi ya Gendarmerie Tnale kwenye mchezo wa kombe la Shirikisho barani Afrika, kutoka katika kikosi ambacho kilicheza na Azam kwenye michuano ya ligi.

Kama ilivyokuwa katika kikosi kilichocheza na Azam, Yusuf Mlipili ameendelea kuaminika na amechaguliwa kuanza pamoja na Shomari Kapombe na Erasto Nyoni katika safu ya ulinzi ambayo leo watacheza mabeki watatu.

Katika nafasi ya kiungo kocha Lechantre amekuja na mfumo ule ule kwa kujaza wachezaji watano ambao ni pamoja na James Kotei, Asante Kwasi, Said Hamis Ndemla, Jonas Mkude pamoja na Shizya Kichuya.

Aidha Mganda Juuko Murushid ambaye alikosekana katika michezo kadhaa kutokana na kuumwa Malaria amewekwa benchi nap engine kutokana na mipango ya mwalimu akaingia baadae ili kuweza kuimarisha safu ya ulinzi.

Kinachoanza: Aish Manula, Shomari Kapombe, Asante Kwasi, Yusuf Mlipili, Erasto Nyoni, Shizya Kichuya, Said Hamis Ndemla, Emmanuel Okwi, John Bocco na Jonas Mkude.

Akiba: Emmanuel Mseja, Mzamiru Yassin, Mwinyi Kazimoto, Moses Kitandu, Paul Bukaba, Ally Shomari na Juuko Murushid.

Mchezo huo unafanyika jioni hii katika uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam, ambapo Simba watahitaji kushinda mabao mengi ili kujihakikishia nafasi ya kucheza hatua inayofuata na mshindi wa mchezo kati ya Green Buffaloes ya Zambia au El Masry ya Misri licha ya El Masry kushinda kwa mabao 4-0 katika mchezo wa kwanza uliofanyika Jumamosi Februari 10.